<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><hymn_number>92</hymn_number>
<title>Nataka Nimjue Yesu TZR92</title>
<lyrics>[V1]
 Nataka nimjue Yesu,
 Na nizidi kumfahamu,
 Nijue pendo lake, na
 Wokovu wake kamili.

[V2]
 Zaidi, zaidi,
 Nimfahamu Yesu,
 Nijue pendo lake, na
 wokovu wake kamili.

[V3]
 Nataka nione Yesu,
 Na nizidi kusikia,
 Anenapo kitabuni,
 Kujidhihirisha kwangu.

[V4]
 Nataka nifahamu, na
 Nizidi kupambanua
 Mapenzi yake, nifanye
 Yale yanayompendeza.

[V5]
 Nataka nikae naye,
 Kwa mazungumzo zaidi,
 Nizidi kuwaonyesha
 Wengine wokovu wake.</lyrics>
</song>